KNUT hatimaye chakubali mtaala mpya

Chama cha taifa cha waalimu-KNUT kimelegeza msimamo wake kuhusu mtaala mpya wa masomo unaozinduliwa na serikali baada ya kudai hapo awali kwamba mtalaa huo hauwezi kutekelezwa na unaharakishwa. Chama cha KNUT kimebadili msimamo baada ya waziri wa elimu Dkt. Fred Matianga��i kuandaa mkutano jana asubuhi la wadau wa sekta ya elimu alipotoa ufafanuzi kuhusu utekelezaji shwari wa mtalaa huo mpya wa masomo. Katibu mkuu wa chama cha KNUT, Wilson Sossion, alisema ameridhika na utaratibu huo na sasa anawahimiza waalimu kujifahamisha mtaala huo ili waweze kuutekeleza kwa uadilifu.

Haya yanajiri baada ya waziri wa elimu kupuuzilia mbali madai kwamba utekelezaji wa mtaala huo mpya wa masomo unakumbwa na changamoto. Kulingana na waziri awamu wa pili ya uzinduzi wa mfumo wa elimu wa 2-6-3-3-3 unatarajiwa kutekelezwa katika shule elfu-33 mwaka huu na mfumo wa elimu wa 8-4-4 utaondolewa kabisa kufikia mwaka wa 2027.

Waalimu elfu-170 wamepokea mafunzo kuhusu mfumo huo mpya wa elimu. Mfumo huo mpya pia utaondolea mbali gredi ya P1 ya kutoa mafunzo kwa waalimu na badala yake kuzindua cheti cha Diploma. Wakati huo huo Matianga��i alitangaza kutolewa kwa shilingi bilioni 29 kwa mipango ya elimu bila malipo inayofadhiliwa na umma katika shule za msingi na upili.