KNCHR Yapinga Matokeo Ya Usajili Wa Polisi Lilofanyika Katika Taasisi Ya NYS

Tume ya kitaifa A�kuhusu haki za binadamu (KNCHR), imetoa wito wa kufutiliwa mbali kwa matokeo ya zoezi la usajili wa makurutu wa polisi lililofanyika katika makao makuu ya shirika la huduma za vijana kwa taifa NYS, ikisema zoezi hilo halikufanyika kwa njia ya haki. Wakiongea na wana-habari katika afisi za KNCHR, Jijini Nairobi, makamishna wa tume hiyo wakiongozwa na mwenyekiti Kagwiria Mbogori walisema makao makuu ya NYS yaliripoti kuhusu visa vya utoaji hongo ambapo makurutu hao walihitajika kulipa shilingi elfu-70 kabla ya kupokea barua za mwaliko wa kujiunga na chuo cha mafunzo ya polisi. Aidha, tume hiyo ilitilia shaka nyakati za kufunguliwa na kufungwa kwa kituo hicho ikisema kituo cha NYS kiliendelea na zoezi la usajili wa makurutu wa polisi hadi usiku. Kulingana na Mbogori, mchunguziA� mmoja wa tume ya KNCHR aliripoti kuwa ukaguzi wa makuruti hao ulifanyika hadi saa kumi na moja na dakika 54 jioni, licha ya ukweli kwamba zoezi la usajili lilitarajia kuwa limesitishwa wakati huo. Mbogori aliishtumu pia Idara ya polisi kwa kujaribu kuwanyima maafisa wa tume ya KNCHR nafasi ya kushiriki kama wachunguzi katika vituo mbali mbali, akisema hiyo ni ishara ya jaribio la kutokuwa na uwazi na wuajibikaji.