KNCHR yadai Kenya inakiuka haki za binadamu

Tume ya kitaifa ya haki za binadamu nchini imesema kuwa Kenya bado inakiuka haki za binadamu hasa katika idara za serikali zinazoongozwa na maafisa wa polisi na kijeshi . Katika ripoti yake kwa rais Uhuru Kenyatta, tume hiyo ililalamika kuwa wananchi hasa wale wanaoshukiwa kuwa na ushirikiano na makundi ya kigaidi wamekabiliwa na ukiukaji wa haki zaoA� kama vile kukamatwa kiholela , kuzuiliwa kinyume cha sheria , mateso, mauaji na kutoweka . Mwenyekiti wa tume hiyo ya kutetea haki za binadamuA� Kagwiria Mbogori sasa anatoa wito kwa rais wakati wa hotuba yake kwaA� taifa kuwaagiza maafisa wa usalama kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria .