KMPDU Kutafuta Msaada Wa Bunge Kuhusu Nyongeza Ya Mshahara

Chama cha madaktari na wataalamu wa meno KMPDU sasa kinatafuta msaada wa bunge ili kutatua mzozo unaoendelea kuhusu nyongeza ya mshahara ambao umedumu kwa miezi miwili sasa. Katika taarifa iliyosomwa na naibu wa spika wa bunge la taifa, daktari Joyce LabosoA�na kutiwa saini na katibu mkuu wa chama cha KMPDU, daktari Ouma Oluga, madaktari wamesema kwamba badala ya kuzingatia utaratibu wa pamoja wa kushauriana na kuafikiana kuhusu jinsi ya kutatua mzozo huo, serikali ya taifa na zile za kaunti zimeamua kuwatisha madaktari kupitia mahakama na tume ya kushughulikia mishahara hapa nchini. Madaktari wanataka bunge la taifa lianzishe utaratibu wa bunge wa kutoa malipo hayo yaliyoafikiwa kwenye mkataba wa mwaka 2013 kama msaada wa masharti kutoka kwa serikali ya kitaifa na zile za kaunti. Aidha chama hicho pia kinataka bunge la taifa lisaidie katika kubuni halmashauri ya huduma za afya ili kushughulikia mizozo ya wafanyikazi wa sekta ya afya yakiwemo maswala ya ugavi wa kazi, mafunzo, mishahara na uhamisho miongoni mwa mengine. Ombi hilo liliwasilishwa kwa kamati ya bunge kuhusu afya ili kujadiliwa na wadau kabla ya kuwasilisha ripoti bungeni. A�Jaribio la mbunge wa Kikuyu, Kimani Ichunga��wa la kupinga ombi hilo kwa kigezo kwamba linashughulikiwa na mahakama, lilipingwa na naibu huyo wa spika.A� A�