Kiunjuri amshtumu Raila akisema anataka kuitumbukiza nchi hii kwenye michafuko

Waziri wa ugatuzi Mwangi Kiunjuri amemshtumu mgombea uchaguzi wa muungano wa NASA, Raila Odinga akisema anataka kuitumbukiza nchi hii kwenye michafuko. Akiongea katika eneo la Mororo kaunti ndogo ya Tana-kaskazini, Kiunjuri alishtumu msimamo mgumu wa Raila kuhusu marekebisho ya mfumo wa uchaguzi kabla ya marudio ya uchaguzi wa urais tarehe 26 mwezi ujao. Kadhalika alikashifu maandamano dhidi ya tume ya IEBC yanayonuiwa kumuondoa afisa mkuu wa tume ya IEBC, Ezra Chiloba kwa madai ya kuvuruga uchaguzi wa urais tarehe 8 mwezi Agosti. Jana wafuasi wa muungano wa NASA waliandamana dhidi ya tume ya IEBC katika barabara za jiji la Nairobi kufuatia miito ya vinara wao.