Kiungo Wa Ulinzi Stars John Nairuka Atarajiwa Kujiunga Na Posta Rangers

Kiungo wa Ulinzi Stars John Nairuka anatarajiwa kujiunga na Posta Rangers wakati wa kipindi cha uhamisho cha katikati mwa msimu kitakachoanza Jumatano juma lijalo.
Nairuka aliyejiunga na Ulinzi Stars mwezi Juni mwaka 2014 kutoka Thika United amekuwa nguzo muhimu kwa kikosi hicho cha kocha Robert Matano. Kandarasi yake na kilabu hicho itakamilika mwezi Juni mwaka huu huku ripoti zikidai kuwa tayari mchezaji huyo ameafikia makubaliano na kilabu cha Posta Rangers. Hata hivyo, kiungo huyo atalazimika kungangania nafasi na aliyekuwa mchezaji wa kimataifa wa Kenya Jerry Santos, Duncan Otieno, Joseph Mbugi, na Moses Otieno. Nairuka alianza taaluma yake katika chuo cha mafunzo ya soka cha a�?NYTAa�� kabla ya kujiunga na Thika United kisha Ulinzi Stars.