Kiungo wa Manchester City Yaya Toure abadili msismamo wake wa kustaafu

Kiungo wa Manchester City Yaya Toure amebadili msimamo wake wa kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Kodivaa.Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 alistaafu kuichezea timu ya taifa ya Kodivaa mwezi September mwaka jana baada ya kuichezea zaidi ya mechi mia moja na pia kutwaa ubingwa wa barani Afrika mwaka 2015. Toure, aliyejiunga na Manchester City kutoka Barcelona mwaka 2010, amecheza mechi tatu pekee za ligi kuu ya soka nchini Uingereza msimu huu. Kodivaa ilishindwa kufuzu kwa fainali za kombe la dunia zitakazoandaliwa mwaka ujao nchini Urusi lakini itaanza kampeini ya kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa bingwa barani Afrika mwezi Machi mwaka ujao.