Kiraitu apuzilia mbali umaarufu wa NASA Meru

Seneta wa kaunti ya Meru Kiraitu Murungi amepuuzilia madai eti muungano wa NASA unaendelea kupata umaarufu katika kaunti hiyo. Akiongea katika sehemu ya Kairia,eneo bunge la Imenti Kusini ,Kiraitu alisema eneo la Meru ni ngome ya Jubilee,ikizingatiwa miradi ya maendeleo rais UhuruA� Kenyatta na naibu wake William Ruto wametekeleza katika sehemu hiyo kwa lengo la kuinua hali ya maisha ya wakazi.Seneta huyo alidai kuwa ziara za hivi punde za vinara wa NASA,wakiongozwa na mgombeaji wao wa urais Raila Odinga katika eneo hilo hazitabadili kisiasa msimamo wa wakazi wa eneo hilo.

Aidha seneta huyo alisema rais Kenyatta atashinda uchaguzi mkuu ujao katika raundi ya kwanza kwa kupata asilimia 70 ya kura .Viongozi wa NASA wanatarajiwa kufanya kampeni katika kaunti ya Tharaka Nithi siku ya Ijuma kabla ya kuelekea Meru siku ya jumamosi kujipia debe .