Kipa Wa Uganda Cranes David Onyango AwapaTumaini Wasimamizi

Wasimamizi wa timu ya Uganda Cranes wana matumaini kwamba mlindalango Denis OnyangoA� atakuwa amepata nafuu kiasi cha kushiriki katika mechi ya ufunguzi ya fainali za mwaka huu za kombe la bara Afrika dhidi ya Ghana uwanjani Stade de Port Gentil tarehe 17 mwezi huu.A� Mlinda lango huyo anayeichezea Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini alijeruhiwa kiuno katika dakika ya 38 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Kodivaa jana. Onyango alijiunga na kambi ya Cranes Jumamosi iliyopita jijini Dubai kutoka Abuja, Nigeria ambako alitangazwa mchezaji bora wa mwaka, anayecheza soka barani Afrika baada ya kuafikia matokeo bora kilabuni na pia katika timu ya taifaA� mwaka jana. Mchezaji huyo anatarajiwa kutekeleza jukumu muhimu kusaida timu ya Cranes, inayoshiriki katika fainali za kombe la bara Afrika kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1978, kuafikia matokeo bora. Uganda itachuana naA� MisriA� tarehe 21 mwezi huu uwanjani Stade de Port GentilA� kisha imalize udhia naA� Mali katika mechi yao ya mwisho yaA� kundi a�?Da�� tarehe 25 mwezi huu.

A�