Kiongozi wa upinzani Russia ahukumiwa

Kiongozi wa upinzani nchini Russia  Alexei Navalny amehukumiwa kifungo cha nyumbani  cha siku 30  kwa kurudia kosa la kuandaa mikutano ya hadhara.Alizuiliwa nyumbani kwake katika mji mkuu ,Moscow jana kabla ya kufanywa maandamano ya kupinga ufisadi nchini humo.Mamia ya waandamanaji wametiwa nguvuni tangu harakati hizo zianze.Mahakama hiyo  ilitoa uamuzi wake jana jioni na kuyakataa madai ya mawakili wa Alexei ya kutaka kesi hiyo  kufutiliwa mbali.Navalny,ambaye anataka kluwania urais mwaka ujao ,alikuwa anatarajiwa  kuhudhuria mojawapo wa mikutano hiyo ya hadhara mjini Moscow ambayo imetangazwa kuwa haramu.