Kiongozi Wa Timu Ya Kenya Ya Olimpiki Stephen Soi Kujibu Mashtaka Leo

soi
Kiongozi wa timu ya Kenya iliyoshiriki kwenye michezo ya Olimpiki jijini Rio Stephen Soi anatarajiwa kufika mahakamani leo kujibu mashtaka ya wizi, utumizi mmbaya wa mamlaka yake na kuwatesa wanamichezo wa Kenya walioshiriki kwenye michezo ya Olimpiki iliyokamilika tarehe 21 mwezi huu nchini Brazil. Soi atakuwa afisa wa tatu wa kamati ya Olimpiki humu nchini a�?NOCKa�� kufika mahakamani baada ya Paul Francis na Pius Ochieng kufanya hivyo siku ya Jumatatatu huku wakiachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki mbili kila mmoja, uchunguzi unapoendelea.

Soi hakufika mbele ya mahakama siku hiyo kwasababu alikuwa amelazwa hospitalini. Watatu hao pamoja na maafisa wengine wa kamati ya NOCK wamejipata katika hali hiyo baada ya timu iliyoshiriki kwenye michezo ya Olimpiki kulalamika kuhusu ukosefu wa mavazi ya wadhamini, shida za usafiri na vibali vya kuingia katika sehemu za wanariadha huku watu wasiojulikana wakijivunia vibali hivyo. Ochieng na FK Paul watafika tena mahakamani tarehe 19 mwezi ujao.