Kiongozi Wa CORD Raila Odinga Asema Nchi Hii Inahitaji Maombi Ili Kukabiliana na Changamoto

Kiongozi wa muungano wa CORD Raila Odinga amesema nchi hii inahitaji maombi kukabiliana na changamoto nyingi zinazoikumba. Akiongea katika kanisa la kiangilikana la Mombasa Memorial wakati wa ibada ya jumapili, Raila alisema ni Mungu pekee anaweza kuinusuru nchi hii kutoka kwa changamoto nyingi zinazoikumba. Alisema ufisadi na migawanyiko ya kikabila ndiyo tisho kuu kwa uthabiti wa nchi hii na kwa mara nyingine akasema ipo haja ya kuandaa kikao cha kitaifa kujadili na kutafuta suluhisho kwa changamoto hizo. Odinga alisema upinzani utaanda sherehe zake za Madaraka katika uwanja wa uhuru park na kuzungumuza kuhusu changamoto zinazokumba nchi hii . Alisema madhumuni ya Cord katika kushinikiza marekebisho katika tume ya uchaguzi a��IEBC ni kuhakikisha kuwa chaguzi zijazo zinaandaliwa kwa njia huru na ya haki.