Kiongozi Wa Chama Cha Wanafunzi katika Chuo Kikuu Cha Nairobi Babu Owino Afikishwa Mahakamani

Kiongozi wa chama cha wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi, Babu Owino leo alifikishwa mahakamani akishtakiwa kwa kumdhuru mkinzani wake, Mike Jacobs. Owino alikanusha madai ya kumchapa Jacobs katika eneo la Kileleshwa jjiinu Nairobi mnamo mwezi Machi licha ya kutolewa kwa picha zinazodaiwa kumuonyesha akifanya hivyo. hakimu mkuu wa Kibera Tito Gesora aliagiza kuachiliwa kwa Owino ambaye jina lake halisi ni Peter Ogili kwa dhamana ya shilingi elfu-20 au shilingi elfu-200 pesa taslimu. Kwenye picha zilizonakiliwa, inaonekana kana kwamba Owino na wenzake walimchapa Jacobs kwenye kituo kimoja cha petroli jijini Nairobi. Owino alikamatwa jana usiku na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Kilimani ambapo alizuiliwa usiku kuchwa. Owino alitangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa viongozi wa chama cha wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi, hatua ambayo ilisababisha malalamishi kutoka kwa wakinzani wake na ghasia za wanafunzi ambao waliteketeza afisi za chama hicho. Jacobs alikuwa miongoni mwa wanafunzi 33 wa chuo hicho waliofukuzwa shuleni kwa kushiriki katika ghasia hizo na kusababisha uharibifu wa mali.

 

A�