Kiongozi Raila Odinga Atamatisha Ziara Yake Busia

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga alitamatisha ziara yake katika kaunti ya Busia kwa kuishtumu serikali kwa kushindwa kutimiza ahadi zake kwa Wakenya .Akiongea katika eneo bunge la Teso Kaskazini,Raila aliwarai wakazi kumpigia kura wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2017,akisema wakati umewadia kwa Wakenya kupata serikali mbadala itakayojali maslahi yao. Aidha aliwahimiza wakazi wa kaunti hiyo kuhakikisha kuwa chama cha ODM kinashinda viti vyote kwenye uchaguzi mkuu ujao ,tofuati na uchaguzi mkuu uliopita ambapo Jubilee ilishinda viti viwili .Kiongozi huyo wa ODM yuko kwenye ziara ya siku tano magharibi mwa Kenya kuthibiti maasi kutoka eneo hilo, ambalo limekuwa likimuunga mkono. Kutoka Busia,raila ataelekea kwenye kaunti ya Kakamega,ambako anatarajiwa kuhitimisha ziara yake ya magharibi ya Kenya.