Kinyesi Cha Ngombe Kutumiwa Kuleta Bahati Nasibu

Wazazi katika kijiji kimoja jimboni Madhya Pradesh nchini India kwa kawaida huwapaka watoto wao kinyesi cha nga��ombe ili kuwapa bahati na kuwakinga dhidi ya magonjwa. Tambiko hilo hufanywa baada ya sherehe kuu ya kitamaduni ya Wahindi almaarufu Diwali. Majuma machache kabla ya sherehe hiyo, wakazi wa kijiji cha Betul hukusanya kinyesi cha nga��ombe na kuombewa kabla ya kupakwa watoto. Nga��ombe huchukuliwa kuwa kiumbe mtakatifu katika dini ya kihindi na wahindi huamini kwamba kinyesi chake pia kinaweza kutumiwa kama dawa.