Kindiki Kithure Awapongeza Makamishna Wa IEBC Wanaoripotiwa Kueleza Nia Ya Kujiuzulu

Kiongozi wa walio wengi katika bunge la Senate Kindiki Kithure amewapongeza baadhi ya makamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipakaA� IEBC ambao wameripotiwa kuelezea nia ya kujiuzulu kabla ya kutekelezwa kwa marekebisho yanayotarajiwa kufanywa katika tume hiyo. KindikiA� ambaye alikuwa akiongea katika shule ya upili yaA� Kajuki katika kaunti ya Tharaka Nithi hata hivyo alisema kuwa makamishna ambao wako tayari kuchunguzwa na kamati ya pamoja ya wanachama 14 inayojumuisha wabunge kutoka muungano tawala waA� Jubilee na mrengo wa upinzani CORD wanapaswa kupewa nafasi ya kujitetea.

Yusuf Nzibo, Albert Bwire, Kule Galma Godana na Abdullahi Sharawe ndio makamishna wanne ambao wameelezea nia yao ya kutaka kujiuzulu. Alipiouzlizwa ikiwa anaweza kuthibitisha kwamba rais Uhuru Kenyatta amepokea barua za kujiuzulu kutoka kwa makamishna hao wanne , hatibu wa Ikulu Manoah Esipisu wakati wa mkutano wa wana habari leo asubuhi hakuongea kuhusu suala hilo.

Upinzani ukiongozwa na muungano wa CORD umekuwa ukishinikiza kundwa upya kwa tume ya IEBC ukisema tume hiyo haiwezi kuaminiwa kuandaa uchaguzi wenye uadilifu .