Kimbunga cha IMRA chakumba eneo la Florida huko Marekani

Kimbunga cha IRMA kimekumba eneo la kati la jimbo la Florida huko Marekani, kusini mwa mji wa Naples huku ikitahadharishwa kuwa huenda mawimbi ya mafuriko ya maji yakafikia kimo cha futi 15. Kimbunga hicho kikiambatana na upepo mkali uliokuwa ukivuma kwa kasi ya kilomitaA� 169 kwa saa, kilichokumba kisiwa cha Marco, kwenye ufuo wa jimbo la Florida, sasa makali yake yameteremshwa hadi ngazi ya pili ya vimbunga. Zaidi ya nyumba milioni 2.5 katika jimbo hilo zimekosa huduma za umeme, huku sehemu za mji wa Miami zikifunikwa na maji. Kumeripotiwa vifo vya watu 3 katika jimbo hilo kutokana na kimbunga hicho. Kwa mujibu wa kituo cha kitaifa cha utathmini wa vimbunga, kimbunga Irma sasa kinavuma kikielekeaA� mji wa Fort Meyers, kaskaziniA� mwa jimbo hilo. Kimbunga hicho tayari kimesababisha uharibifu mkubwaA� katika visiwa vya Caribean na zaidi ya vifo 28. Jumla ya wakazi milioniA� 6.3 wametakiwa kuhama kutoka maeneo yalioathiriwa jimboni humo. Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza jimbo la Florida kuwa aneo la maafa, ambapo sasa linapokea msaada kutoka serikali kuu ili kuwakimu wahanga waA� janga hilo.