Kimbunga cha Imra chakumba Caribbean

Kimbunga cha Irma kimekumba eneo la Caribbean na kusababisha vifo vya watu-9. Aidha, hali ya hatari imetangazwa katika majimbo ya Florida, Georgia na South Carolina nchini Marekani ambayo yanatarahiwa kukumbwa na kimbunga hicho. Kimbunga hicho kinavuma kwa kasi ya maili-180 kwa saa. Hapo jana, kimbunga cha Irma kiliharibu asilimia-90 ya mijengo na magari katika eneo la Barbuda huku watu wanane wakiripotiwa kufariki na 23 kujeruhiwa katika visiwa vya St Martin na St Barthelemy.