Kimbuga chaangamiza watu 6 Florida ,Marekani

Watu sita katika kituo kimoja cha afya katika jimbo la Florida kilichoachwa bila nguvu za umeme kwa siku kadhaa baada ya kimbunga  Irma wamefariki. Polisi waliwaokoa watu  115 kutoka kituo hicho siku ya Jumatano ambao uyoyozi wao ulikatizwa kutokana na kimbunga hicho . Meya wa kaunti ya Broward Barbara Sharief  alisema watu watatu walipatikana wamefariki katika kituo hicho cha afya katika mji wa  Hollywood. Wengine watatu walifariki katika hospitali hiyo . Watu milioni 10 bado wanaisha bila nguvu za umeme katika Majimbo ya Florida, Georgia na Carolina baada ya kimbunga  Irma.