Kimanzi Ateuliwa Kocha Bora Wa Mwezi

Kocha Wa Mathare United Francis Kimanzi ametua tuzo la Sports Journalists Association of Kenya (SJAK) Fidelity Insurance Kocha Bora Wa Mwezi Februari 2016.

Kimazi alipata alama 21A� ya kura zilizopigwa na kamati ya kandanda ya SJAK na kuwabwaga wenzake Odijo Omondi (17) wa Muhoroni Youths na Zedekiah Zico Otieno (16) wa Posta Rangers.

Tuzo hilo linaambatana na kitita cha Ksh 50 000 na kombe la kipekee. Kocha huyo alishukuru SJAK na wachezaji wake kwa kumuezesha kutua taji hilo.

a�?Nashukuru SJAK na klabu changu kwa tuzo hili. Wachezaji na wasaidizi wangu wamefanya kazi bora. Nina wakufunzi walio na uwezo tosha na wanafanya kazi nzuri, Kimanzi yu hapa haswa kuleta mbinu na ujuzi zaidi,a�? alisema Kimanzi.

Kwa muda wa mwezi mmoja Kimanzi ameandikisha ushindi mara mbili na sare mara moja.