Kim Jong-un kusitisha utengenezaji wa zana za nyukilia

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ameahidi kusitisha utengenezaji wa zana za nyukilia.Kim jong alisema hayo wakati wa mkutano wake wa kwanza na rais wa China Xi Jinping mjini Beijing.Shirika la habari la Xinhua limemnuku kiongozi huyo wa Korea Kaskazini akisema yuko tayari kusimamisha ustawishaji wa zana za kivita ikiwa Korea Kusini na Marekani zitaonyesha nia njema na kujitolea kwa vitendo kusuluhisha tofauti zilizopo. Aidha Kim amenukuliwa akisema hana shida kukutana na rais wa Marekani A�Donald Trump. Hiyo nduyo ziara ya kwanza ya Kim nje ya Korea Kaskazini tangu alipochukua mamlaka mnamo mwaka 2011.