Kilo mbili ya unga yashuka bei hadi shillingi tisini

Kuanzia leo tarehe 17 utaweza kununua pakiti ya kilo mbili ya unga wa mahindi kwa shillingi tisini na pakiti ya kilo moja ya unga huo kwa shilling 47.Waziri wa kilimo Willy Bett amesema bei hizo mpya ziliafikiwa baada ya mashauri ya kina na wasagaji unga wa mahindi.Akiongea na wanahabari waziri alisema serikali itatumia shilingi bilioni sita kufidia bei ya unga kwani wasagaji mahindi wa hapa nchini sasa watanunua gunia moja la mahindi kwa shilingi 2,300 kutoka shillingi 4,620.Waziri alisema serikali inapanga kuagiza mahindi kutoka Zambia na Ethiopia lakini akaongeza kusema kwamba jukumu la kuagiza mahindi hayo limeachiwa kampuni za kibinafsi za kusaga mahindi.Serikali inasisitiza kwamba ina magunia elfu 980,ya mahindi hapa nchini yatakayotumika hadi tarehe 29 mwezi huu ilhali waagizaji mahindi wa ikibinafsi wahatarajiwa kuagiza magunia mengine million 2.1 ya mahindi mwezi ujao na mengine million tatu mwezi julai kabla ya msimu wa mavuno ya mahindi kuwadia.Waziri alijitetea dhidi ya shutuma za kuipotosha nchi hii kwa matamshi aliyotoa mwezi agosti mwaka uliopita eti kuna chakula cha kutosha hapa nchini na nchi hii haitahitaji kuagiza mahindi zaidi.