Kilio Cha Wakulima Katika Eneo La Mwingi

Wakulima katika eneo la Mwingi, kaunti ya Kitui wanakadiria hasara baada ya wachungaji wa mifugo wanaoshukiwa kutoka jamii ya Wasomali kuvamia mashamba yao karibu na mpaka kati ya kaunti zaA� Kitui na Tana River.

Kisa hicho cha hivi punde huenda kikasababisha utovu wa usalama kwani ni mwaka uliopita tu ambapo watu wanne kutoka kaunti ya Kitui waliuawa na wachungaji wa mifugo waA� kisomali walipojaribu kuwazuia kulisha ngamia kwenye mashamba yao.

Wakazi wa kijiji cha Ukasi wamesema waliamka na kupata kundi la ngamia kwenye mashamba yao na walipojaribu kuwauliza wachungaji hao walisema ardhi ni ya umma na hawatazuiwa kulisha mifugo yao kwenye ardhi hiyo. Wakazi hao sasa wametoa wito kwa serikali kuwasaidia.