Kilemi Mwiria Ajiunga Na Chama Cha Maendeleo Chap Chap

Waziri msaidizi wa zamani wa elimu Dr. Kilemi Mwiria amejiunga na chama cha gavana wa Machakos Alfred Mutua chaA� Maendeleo Chap Chap baada ya kukihama chama cha Jubilee kuwania kiti cha ugavana cha Meru. Akiongea hapa jijini Nairobi Dr. Mwiria ambaye ni mshauri maalum wa Rais Uhuru Kenyatta kuhusu maswala ya elimu alisema ameamua kujiunga na chama cha Maendeleo Chap Chap kwa sababu kinazingatia maendeleo ya demokrasia ambayo wakenya wanataka. Alisema anatumai kwamba atashinda kiti cha ugavana cha Meru kwa tiketi ya chama hicho wakati wa uchaguzi mkuu hapo Agosti 8. Dr. Mutua alimkaribisha chamani akimtaja kuwa mtu mwaminifu, mkarimu na kiongozi anayependa maendeleo.Aidha Mutua alitangaza kwamba chama cha Maendeleo Chap Chap kitakuwa na wagombea katika kaunti zote kwa viti vya uchaguzi isipokuwa kiti cha urais kwa vile chama hicho kitamuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta kuchaguliwa tena.Dr. Mwiria na seneta wa Meru Kiraitu Murungi wamesema watawania kiti hicho ili kumuondoa gavana wa sasa wa Meru Peter Munya.