Keter Azungumzia Mipango Ya Serikali Kusambaza Nguvu Za Umeme Manyumbani

Waziri wa kawi Charles Keter amesemaA� kuwa serikali inapanga kusambaza nguvu za umeme katika nyumba milioni 2 kufikiaA� mwakaA� ujao. Akiongea katika shule ya msingi yaA� Thange alipoenda kufungua rasmi shughuli ya kusafisha mto Thange kufuatia kumwaika kwa mafuta katika kaunti ndogo ya Kibwezi Mashariki, keter alisema kuwa kuna mradi utakaoanza mwezi ujao na anatumaini kuwa nyumba zote nchini zitakuwaA� na nguvu za umeme kabla ya mwisho wa mwaka ujao. Waziri huyo alisema kuwaA� shule nyingi zitakuwa na nguvu za umeme ili kuafikia ahadi zilizotolewaA� na serikali.A� Wakati huo huo, Keter alivionya vituo vya petroli vinavyochanganya dieseli na mafuta taa kuwa watakabiliwa kisheria. Waziri huyo alikuwa akizungumzia kilio chaA� wananchi kuhusu madai kuwaA� baadhi yaA� vituo vya mafutaA� katika miji yaA� Mtito Andei na Kibwezi Vinatekeleza biashara hiyo haramu.