Kesi ya kupinga uchaguzi wa mbunge wa kisauni yatupiliwa mbali

Mahakama kuu huko Mombasa imetupilia mbali kesi inayopinga uchaguzi wa mbunge wa Kisauni Ali Mbogo kwenye uchaguzi mkuu wa agosti 8 mwaka uliopita kwa sababu ya ukosefu wa ushahidi.Mlalamishi,aliyekuwa mbunge wa eneo hilo Rashid Bedzimba ameagizwa kulipa shilingi million 2.5 za gharama ya kesi hiyo .Katika uamuzi wake,jaji Erick Ogola alisema hakuna ushahidi wa kuthibitisha kwambaA� uchaguzi huo haukuwa wa haki na kuaminika .Akiongea na waandishi wa habari baada ya uamuzi wa mahakama,Mbogo alisema ameridhika na uamuzi huo na kuwaalika wapinzani wake kuungana naye kutekeleza maendeleo kwa manufaa ya wakazi wa eneo bunge hilo.