KERRA kutoa mafunzo kwa waendeshaji magari

Kwingineko halmashauri ya kushughulikia barabara za mashambani hapa nchini (KERRA) kwa ushirikiano na halmashauri ya kitaifa kuhusu uchukuzi na usalama barabarani zimeandaa shughuli ya utoaji mafaunzo kwa waendeshaji magari kwenye hafla iliyoandaliwa katika eneo la Chepnyogaa, kaunti ndogo ya Belgut kaunti ya Kericho . Afisa mkuu wa polisi huko Kericho Michael Kahara ametoa wito kwa waendeshaji magari wakiwemo wahudumu wa bodaboda kuhakikisha kuwa wana leseni za kuhudumu na kufuata kanuni za trafiki kila wakati. Isaac Selali, ambaye ni msimamizi wa halmashauri ya NTSA katika kaunti za Kericho na Bomet amesema mtaala mpya wa uendeshaji magari ambao utaanza kutekelezwa mwezi Januari utawezesha kubuniwa kwa leseni za dijitali za uendeshaji magari ambazo zitanakili maelezo yote ya madereva. Wakati wa shughuli hiyo wahudmumu wa bodaboda wanaotumia barabara ya Kabianga-Premier hata hivyo walilalamika kuhusu madai ya polisi kushinikiza kupewa hongo.