Keriako Tobiko azindua kampeni ya kitaifa ya upanzi wa miti

Waziri wa mazingira Keriako Tobiko amezindua kampeini ya kitaifa ya upanzi wa miti inayolenga kuongeza marudufu eneo la misitu nchini kutoka kiwango cha sasa cha asili mia saba hadi asili mia 15 kufikia mwaka 2022. Akiwahutubia wanahabari baada ya kuongoza hafla ya upanzi wa miti kwenye msitu wa Ngong , Tobiko alisema serikali A�huenda ikatenga siku ya kitaifa ya upanzi wa miti katika juhudi za kuwahamasisha wakenya kuhusu uhifadhi wa misitu.Tobiko aliongeza kuwa ili kutimiza pendekezo la umoja wa mataifa la kuwa na eneo la misiti wa asili mia kumi nchini,takriban miti milioni moja zitahitaji kupandwa kila mwaka katika kaunti zote 47.

Kampeini hiyo ya upanzi wa miti inafuatia uzinduzi wa jopo kazi la kuchunguza upya usimamizi wa misito kote nchini.Jopo kazi hilo linatarajiwa kupendekeza hatua zitakazochukuliwa kuhakikisha kuwa takriban ekari nusu milioni za chemichemi za zinanusuriwa kupitia upanzi wa miti. A�