Kenyatta Asema Amechukua Hatua Kukabiliana Na Ufisadi.

Rais Uhuru Kenyatta leo ametetea serikali yake dhidi ya madai kuwa imeshindwa kukabiliana na ufisadi hapa nchini. Akiongea leo asubuhi katika ikulu ya Nairobi wakati wa kongamano kuhusu ufisadi raisA� Kenyatta alisema serikali yake imefanya vyema katika kukabiliana na ufisadi kuliko serikali zote zilizotangulia. Rais alisema amechukua hatua zote zilizoratibishwa kwenye katiba kupambana na ufisadi. Rais aliwapa changamoto maafisa wa serikali waliojukumiwa kupambana na ufisadi kufanya kazi yaoA� ipasavyo. Wakati huo huo rais aliwataka wanasiasa kukoma kutumia maswala ya ufisadi kwa manufaa yao ya kisiasa na kuvitaka vyombo vya habari kuwashinikiza wale wanaotuhumu wengineA� kwa ufisadi kutoa ushahidi.

Aidha rais alisema atawaachiliaA� wafungwa wanaotumikia vifungo gerezani kwa makosa madogo ili kutoaA� nafasi kwa washukiwa wa ufisadi katika magereza.

Kuhusu matamshi yaliyozua utata ya seneta wa kaunti yaA� Nairobi Mike Sonko rais aliwataka wakenya kupuuza yale yanayosemwa katika ibada za mazishi akisema akiwa nje au ndani ya nchi yeye angali rais wa taifa hili.