Kenyatta Aonya Upinzani Dhidi Ya Kuzua Ghasia

Rais Uhuru Kenyatta amesema kwamba serikali iko tayari kuhakikisha kwamba hakuna mkenya atakayejeruhiwa au mali kuharibiwa kwasababu ya uchaguzi. Akijibu vitisho vya Raila Odinga na washirika wake wa kisiasa kwamba watazua ghasia hapa nchini baada ya uchaguzi, rais alisema serikali iko tayari kushughulikia jaribio lolote la kuzua ghasia. Rais alisema upinzani unazungumza mara kwa mara kuhusu kuzua ghasia hapa nchini badala ya kuangazia jinsi wanavyoweza kuwashawishi wakenya kuwapigia kura. Aliwakashifu viongozi wa upinzani kwa kutokuwa na maono kwa taifa hili. Rais aliongeza kuwa ingawa upinzani unawachochea wakenya, matusi wanayotoa kila siku yanawadhihirishia wakenya kwamba hawafai kuwa viongozi. Rais ambaye alikuwa akiongea huko Kiritini katika kaunti ya Embu wakati wa kampeni ya kuwahamasisha wakazi kusajiliwa kuwa wapigakura, alisema serikali ya Jubilee haiko tayari kujihusisha na mambo madogo madogo ambayo upinzani unazungumzia. A�Rais alitoa wito kwa wakenya wawapinge wale wanaozua taharuki na kuchochea ghasia. Aliwahimiza wakazi wa kaunti ya Embu kusajiliwa kwa wingi kuwa wapigaji kura ili washiriki katika uchaguzi mkuu ujao. A�