Kenya Yaimarisha Uhusiano Wa Kibiashara Na Uingereza

Kenya na Uingereza zimekariri kujitolea kwao kuimarisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji badala ya kutegemea misaada. Kwenye mkutano baina ya naibu rais,A�William Ruto na balozi wa Uingereza hapa nchini, Nic Hailey katika eneo la Karen, ilibainika kuwa uhusiano huo utasababisha kunawiri wa sekta za kawi, muundo mbinu, klilimo na maji.A�Ruto alihimiza kampuni za Ungereza kuwekeza katika sekta ya kawi hapa nchini hususan kawi inayotokana na mvuke wa ardhini na pia katika uchimbaji mafuta. Alisema kunaA�fursa nyingi za uwekezaji katika sekta ya kilimo ambazo kampuni za Uingereza zinaweza kuweka vitega uchumi ili kuimarisha uzalishaji chakula.A�Viongozi hao walikubaliana kwamba Uingereza inaweza kutekeleza jukumu muhimu katika juhudi za serikali za kuimarisha bandari ya Mombasa.A�Ruto alisifu kampuni za Uingereza kwa kuwekeza katika sekta za utalii, benki, majani chai, kahawa na kilimo cha mboga na matunda hapa nchini hali ambayo inaweza kuimarishwa zaidi kupitia uwekezaji katika nyanja za utayarishaji bidhaa za kilimo