Kenya Power yapunguza gharama ya umeme kwa wenye biashara

Kampuni ya umeme, Kenya Power imepunguza gharama ya umeme kwa wenye biashara kubwa na viwanda mwishoni mwa juma kwa nia ya kuwavutia wawekezaji na kupunguza bei ya bidhaa. Ada hizo mpya zilichapishwa kwenye gazeti rasmi la tume ya kudhibiti kawi huku taarifa hiyo ikisema hatua hiyo itachangia ustawi wa taifa na kubuni nafasi za ajira. Ada hizo zitatekelezwa siku za Jumamosi na Jumapili na pia sikukuu. Kampuni hiyo pia imepunguza gharama ya umeme kwa wenye viwanda kati ya saa nne usiku na saa kumi na mbili alfajiri.