Kenya na Ushelisheli zatia saini mikataba muhimu ya kibiashara

Kenya na ushelisheli jana zilitia saini mikataba itakayoziwezesha nchi hizi mbili kuimarisha uhusiano wao wa kibiashara na usalama. Mikataba hiyo iliafikiwa wakati Rais Uhuru Kenyatta aliposhauriana na RaisA� wa ushelisheli anayezuru hapa nchini.Mashauri hayo yaliyoandaliwa katika ikulu ya Nairobi yaliafikia mikataba kadhaa ikiwemo ya kuwapa ajira wakenya nchini Ushelisheli na kuuza mazao ya kilimo nchini humo. Kuhusu Utalii, Rais Faure alisema Kenya na Ushelisheli zimeafikia makubaliano ya kuimarisha utalii kwa pamoja. Rais Kenyatta alisema Kenya na ushelisheli zina vivutio vingi vya watalii na itakuwa manufaa ya kiuchumi iwapo nchi hizi mbili zitashirikiana katika kuimarisha utalii.