Kenya Kushauriana Upya Na Uingereza Kuhusu Mkataba Wa Mazoezi Ya Wanajeshi Nchini

Kenya inatarajiwa kushauriana upya na serikali ya Uingereza kuhusu mkataba wa ushirikiano wa kijeshi unaoruhusu wanajeshi wa Uingereza kuendelea kufanya mazoezi yao hapa nchini. Mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu ulinzi na uhusiano wa kigeni, Ndunga��u Gethenji ameisema mataifa hayo mawili yanatarajiwa kutia saini makubaliano hayo kabla ya kuratibishwa bunge.A�Gethenji amewahimiza wananchi watoe maoni yao kuhusu swala hilo ili yajumuishwe kwenye ripoti itakayowasilishwa bungeni kwa manufaa ya nchi hii. Mbunge huyo wa Tetu ameelezea matumaini yake kwamba wabunge wataidhinisha mkataba huo wa ushirikiano wa kijeshi kati ya Kenya na Uingereza unaoruhusu wanajeshi wa Uingereza kuendelea na maneva zao katika eneo la Nanyuki, Kaunti ya Laikipia.