Kenya Airways kuboresha huduma zake

Mwenyekiti wa shirika la ndege la Kenya Airways, Michael Joseph amesema shirika hilo limechukua hatua nyingine ya kuhakikisha ukuaji wake wa muda mrefu baada ya kukamilisha mpango wake wa kujiimarisha kifedha. Kwenye taarifa kwa vituo vya habari leo , Joseph amesema mpango huo uliwezesha wadau wote muhimu wa shirika hilo kutia saini mkataba wa kujitolea kwao kushiriki katika kuimarisha mstakabali wa shirika hilo. Joseph ametaja mchakato huo kuwa muhimu A�kwani umewaleta pamoja wadau wote muhimu kukubali kulinda mstakabali wa shirika hilo.

Joseph pia amepongeza serikali kwa kutekeleza wajibu muhimu kusaidia shirika hilo wakati lilipokuwa likielekea kusambaratika kutokana na madeni. Mchakato huo wa kuimarisha shirika hilo utawezesha mgao wa serikali kuongezeka kutoka asilimia 29.8 hadi 48.9 . Benki za hapa nchini zina mgao wa asilimia 38.1 . Kampuni ya KLM itakuwa na mgao wa asilimia A�7.8 . Waziri wa fedha A�Henry Rotich amepongeza hatua hiyo na kuahidi kuwa serikali itasaidia kuimarisha shirika hilo la A�Kenya airways. A�