KEMRI Yakanusha Madai Ya Ufisadi

Taasisi ya utafiti wa matibabu hapa nchini-KEMRI imepuuzili mbali madai kwamba ilitia sahihi mkataba wa makubaliano na kituo cha mafunzo na utafiti cha RCTP ambacho kinadaiwa kuhusika katika ufujaji pesa zilizotolewa na wafadhili. Kwenye taarifa, taasisi ya KEMRI imesema haina uhusiano rasmi na kituo hicho. Taasisi ya KEMRI imesema pesa za ufadhili hutolewa kwa mtafiti binafsi ambaye hupewa masharti na wafadhili hao kuhusu matumizi ya pesa hizo. Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari leo asubuhi afisa mkuu mtendaji wa taasisi hiyo, Gerald Mkoji alisema taasisi ya KEMRI hushirikiana na watafiti wengine hapa nchini na wale wa kimatifa kufanya utafiti ambao umefanikisha kubuniwa kwa sera za kudhibiti magonjwa mbalimbali.
Taarifa hiyo imetolewa siku mbili baada ya kuibika kwa madai kwamba mafisa wa kituo cha RCTP walitia sahihi mkataba wa mkubaliano na taasisi ya KEMRI ambapo mamilioni ya pesa zililaghaiwa.