Kaunti zisizoendelea Kunufaika na Bilioni 6

Rais Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa shilingi bilioni-6 zitatumiwa kusawazisha maendeleo katika kaunti zilizobaki nyuma kimaendeleo hapa nchini. Fedha hizo ni asilimia-0.8 ya mapato ya serikali yalioidhinishwa na bunge la taifa huku kiasi hicho kikiongezeka kutoka asilimia-0.5 iliyoratibishwa kwenye katiba.

Alisema kuwa chini ya hazina hiyo,kaunti zilizoko katika maeneo kame zitapokea kati ya shilling million 185 na million 650A� katika kipindi cha mwaka huu cha matumizi ya pesa za serikali.

Rais ambaye alikuwa ameandamana na naibu wake William RutoA� alisema hayo alipofungua mkutano kuhusu uongozi bora kwa jamii za wafugajiA� katika mgahawa wa Simba Lodge katika kaunti ya Isiolo.

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi kutoka kaunti zaA� Isiolo, Mandera, Wajir, Garissa, Marsabit, Turkana, West Pokot, Baringo, Laikipia, Samburu, Tana River, Lamu, Kajiado na Narok.Rais alisema ana imani kwamba pesa za hazina hiyo zikitumika kwa vyema, zitabadilia maeneo hayo kimaendeleo na hivyo kuinua hali ya maisha ya wakazi.