Kaunti ya Mandera yazidi kuadhiriwa na ukame

Zogo la kibinadamu linatokota katika kaunti ya Mandera huku maelfu ya wakazi wakihamia miji mikubwa katika kaunti hiyo kufuatia kukithiri kwa athari za hali ya ukame. Baada ya kupoteza asilimia 90 ya mifugo wao, wafugaji wamejenga mabanda katika juhudi za kutaka kupokea misaada kwenye hatua ambayo imezua upya hali ya wasiwasi kuhusu uwezekano wa kuzuka maradhi yanayoambukizwa kupitia maji machafu na pia mizozo ya kijamii. Haya yanajiri huku serikali na wadau wakiimarisha juhudi za kuwakimu wanaoathiriwa na ukame. Zaidi ya watu milioni tatu wameathiriwa na ukame huku taasisi za kutoa misaada ya kibinadamu zikikadiria kwamba idadi hiyo yaweza kuongezeka hadi watu milioni nne iwapo mvua ya kutosha haitanyesha msimu huu. Anayenuia kuwania kiti cha ubunge cha Mandera kusini, Mohammed Isaac Hassan, sasa ametoa wito wa kutaka misaada ili kuthibiti hali hiyo ambayo imekuwa tisho kwa watu, mifugo na wanyama pori.

SerikaliA�A�imetangaza hali ya ukame inayojiri kwa sasa katikaA�A�sehemu nyingi za nchi kuwa mkasa wa kitaifa.