Kiambu yapongezwa kwa huduma ya dharura ya matibabu licha ya mgomo

Idara ya afya ya kaunti ya Kiambu imepongezwa kwa kutoa huduma za dharura ya A�matibabu licha ya mgomo wa madadkatari unaoendelea.Akiongea katika kijiji cha Maguguni kilichoko kaunti ndogo ya Thika mashariki wakati wa ziara ya nyumbani kwa mgonjwa mmoja wa kifafa aliyegonga vichwa vya habari mwezi Novemba mwaka uliopita baada ya kuanguka kwenye moto A�na kupata majeraha mabaya ya moto, mfanyibiashara mmoja mwanamke wa Thika , Wairimu Muriuki,alimpongeza gavana wa kaunti ya Kiambu William Kabogo A�na idara yake ya afya A�kwa kujitokeza na kumpa matibabu ya dharura A�licha ya mzozo unaoikumba idara ya matibabu.Bi. Muriuki alisema teknolojia ya kisasa ya mawasiliano ilisaidia kuokoa maisha ya Samuel Gitonga A�wakati picha za majeraha yake ziliposambazwa kupitia mitandao ya kijamii zikionyesha masaibu aliyokuwa akipitia baada ya familia yake kushindwa kumpeleka kwa matibabu kwa sababu ya mgomo unaoendelea wa madaktari.Mgonjwa huyo ambaye amekuwa akipokea matibabu kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita aliruhusiwa kuondoka hospitalini wiki iliyopita A�lakini anahitaji kufanyiwa upasuaji wa ngozi punde tu madaktari wanaogoma watakaporejea kazini.