Karua atoa ushahidi katika kesi ya kupinga uchaguzi wa Ann Waiguru

Kiongozi wa chama cha Narcka��Kenya, Martha Karua, leo alisimama kizimbani kutoa ushahidi kwenye kesi inayopinga ushindi wa Ann Waiguru kwenye uchaguzi wa ugavana huko Kirinyagah. Karua alidai uchaguzi wa Ann Waiguru ulikumbwa na kasoro nyingi ambazo zilihujumu uhalali na uadilifu kwenye shughuli hiyo. Kwenye ushahidi wake mbele ya jaji Lucy Gitari, Karua alidai kwamba uchaguzi wa Waiguru ulitokana na habari za kupotosha na kuhangaishwa na kuhongwa kwa wapiga kura na kwamba matokeo ya wagombea uchaguzi hayangebainishwa. Kusikizwa upya kwa kesi hiyo kulianza kufuatia maagizo ya mahakama ya rufaa kwamba kesi hiyo irejelewe kwa misingi kwamba mahakama kuu haikutoa uamuzi ufaao kwa kutupilia mbali rufaa hiyo. Hata hivyo ombi la Karua la kutaka jaji mwingine kusikiza rufaa hiyo halikufua dafu baada ya jaji wa mahakama kuu Lucy Gitari kukataa kujiondoa kusikiza kesi hiyo iliyopinga uchaguzi wa gavana huyo wa Kirinyagah