Karua ataka uchaguzi wote wa tarehe 8 Agosti kufutiliwa mbali

Kiongozi wa Narc-Kenya, Martha Karua amewasilisha kesi ya dharura kwenye mahakamaa ya ki-katiba, akitaka kufutiliwa mbali kwa uchaguzi wote ulioandaliwa tarehe 8 Augosti mwaka huu. Kulingana na mbunge huyo wa zamani wa Gichugu, matokeo ya uchaguzi wa viongoziA� wote nchiniA� kutoka kwaA� Ma-gavana, Ma-seneta, Waakilishi wa wanawake, wa-Bunge na pia Wanachama wa Ma-Bunga yaA� kaunti, unapaswa kufutiliwa mbali. Katika ombi lake mbele ya mahakama kuu ya Kerugoya, waziri huyo wa zamani wa maswala ya ki-katiba alisema kwamba uchaguzi wa Urais uliandaliwa sambamba na ule wa nyadhifa nyingine tano, na hakuna vile matokeo ya uchaguzi wa Urais yangefutiliwa mbali na kuacha yale ya nyadhifa nyingine. Kupitia kwa wakili Gitobu Imanyara, Karua alihimiza mahakama kuwasilisha ombi hilo kwa jaji mkuu, ili aweze kubuni jopo la Ma-jaji watatu la kusikiza swala hilo.

Swala hilo litasikizwa na pande zote husika,A� siku ya Jumatatu tarehe 18 Septemba katika mahakama kuu ya Kerugoya.