Kariuki Mate Ataka Ukaguzi Wa Kina Kufanywa Kuhusu Ununuzi Wa Vifaa Vya Kisasa Vya Matibabu Kwenye Hospitali Ya Embu Level Five

Spika wa bunge la kaunti ya Embu, Kariuki Mate anataka ukaguzi wa kina ufanywe kuhusu ununuzi wa vifaa vya kisasa vya matibabu kwenye hospitali ya Embu level five. Mate ametilia shaka shughuli ya ununuzi wa vifaa hivyo akisema ipo haja ya kubainisha aina ya vifaa vinavyohitajika kwenye hospitali hiyo. A�Alidai kuwa serikali ya kaunti hiyo ilinunua vifaa vitano vya uchunguzi wa kimatibabu vya MRI, vitano vya CT Scan na mashine nyingine kadhaa za kusafisha damu ilihali mashine moja inatosha kwa hospitali hiyo. Alidai kwamba hatua ya gavana wa eneo hilo ya kuharakisha ununuzi wa vifaa hivyo ni njama ya kupora pesa za umma.A�Mate alionya kwamba mashine hizo huenda zisitumike kwani hakuna wataalamu wa kuzitumia.