Karatasi za kura ya urais zatarajiwa kufika hapa nchini leo jioni

Shehena ya kwanza ya karatasi za kura ya urais inatarajiwa hapa nchini leo jioni. Karatasi hizo za kaunti-30 zitapokewa na maafisa wa tume ya IEBC katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta. Karatasi zilizosalia za kura ya urais zinatarajiwa kuwasilishwa kesho jioni. Karatasi hizo zilizochapishwa na kampuni ya Al GurairA�ziko kwenye vijitabu-416,360 huku kila kijitabuku kikiwa na kurasa-50. Ni karatasi milioniA�20,818,000 za kura ya urais zilizochapishwa ikilinganishwa na idadi ya wapiga kura milioni 19 646 673 waliosajiliwa. Hii ni nyongeza ya asili mia moja endapo kutakuwa na kura zinazoharibika. Karatasi hizo zina alama maalum ambayo inaweza tu kuonekana kwa kutumia miale yaA�ultraviolent na pia zina nambari maksus za usajili. Uchapishaji wa karatasi hizo za kura ya uraisA�A�ulianza wiki jana baada ya mahakama ya rufani kuidhinisha tume ya IEBC kuzichapisha karatasi hizo ilipopata ushindi mahakamani kwenye rufaa ya kuzuia kampuni ya Al Ghurair kuchapisha karatasi hizo. Karatasi za kura za Ugavana, Waakilishi wa wanawake na Maseneta tayari zimewasili hapa nchini.