KANU Yapuzilia Mbali Matokeo Ya Uchaguzi Huko Kericho

Chama cha KANU kimepuzilia mbali matokeo ya uchaguzi mdogo wa jana wa useneta huko Kericho kikidai kulikuwa na mapendeleo.

Mgombeaji waA� KANU Paul Sanga�� alidai matokeo ya uchaguzi huoA� mdogo hayakuwiana.A�A� Sanga�� alidai maajenti wake walitimuliwa na maafisa wa tume ya uchaguzi katika baadhi ya vituo vya upigaji kura huko Belgut kwa madai eti hawakuwa maajenti halali.

Kanu pia ilidai maafisa wa usalama pia walikuwa na mapendeleo na sasa kimeahidi kutangaza matokeo sambamba kesho.Hata hivyo seneta mteule wa Kericho Aaron CheruiyotA� akiongea wakati wa kukabidhiwaA� cheti chake cha ushindi,alikanusha madai hayo ya Kanu.

Wakati huo huo,wafuasi wa JAP huko Malindi wakiongozwa naA� Gideon Munga��aro wamekiri kushindwa kwenye uchaguzi huo.Wabunge hao walikariri kwamba watendelea kushirikiana na serikali kabla ya uchaguzi mkuu ujao.