Kansella Angela Merkel achaguliwa tena kwa mara ya nne, Ujerumani

Kiongozi wa Ujerumani Kansella Angela Merkel amechaguliwa tena kwa mara ya nne kuongoza taifa hilo, huku chama cha itikadiA� kali zaA� uzalendo kikijipatia ushindi wa kihistoria kwenye uchaguzi huo. Hata hivyo muungano wa vyama vya CDU na CSU unaoongozwa na Merkel haukupata uungwaji mkono mkubwa ilivyotarajiwa, japo utasalia kuwa na wajumbe wengi bungeni. Mshirika wa muungano huoA� wa chama cha kisoshalisti cha SDP, umesema kuwa utajiunga na upinzani baada ya kupata pigo kwenye uchaguzi huo. Chama kinachofwata siasa za mrengo wa kulia chaA� AFD kilijipatia ushindiA� muhimu na kuibuka cha tatu kwenye uchaguzi huo. Kilijipatia ushindi huo kutokana na sera zake za kupinga uislamu na kitakuwa naA� viti bungeni kwa mara ya kwanza. Matokeo ya awaliA� yalionyesha kuwaA� chama cha SDP kinachoongozwa na Martin Schulz kilipata kura chache mnoA� tangu vita vikuu vya pili vya dunia. Alisema kuwa matokeo hayo yanamaanisha mwisho wa ushirikiano na muunganoA� wa Merkel, ambaye hana budi sasa kubuni muungano mpya, jambo litakalochukua miezi kadhaa. Imearifiwa kuwaA� huenda kukawa na vyama sita vikuu vya kisiasaA� katika bunge la sasa tangu vita vikuu vya pili vya dunia.