Kanisani la Katoliki Austiralia lakataa pendekezo la kuripoti visa vya dhuluma za kimapenzi wahusika wakikiri makosa yao

Kanisa katoloki nchini Australia limekataa pendekezo la jopo la uchunguzi la kuwataka makasisi kulazimishwa kuripoti visa vya dhuluma za kimapenzi baada ya waliohusika kukiri makosa yao.

Uchunguzi huo uliodumu kwa miaka mitano umedokeza kuwa maelfu ya watoto walidhulumiwa katika taasisi kadhaa nchini Australia huku visa vingi vikiripotiwa katika kanisa katoliki. Hata hivyo kanisa hilo limekubali mapendekezo mengine ya jopo likisema swala la toba huenda likazua mzozo na serikali.

Baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini Australia limesema udokezi wa kanuni za toba ni kinyume cha imani na maadili ya kanisa hilo. Wanasema kuwa wamejitolea kulinda watoto na watu wengine walio kwenye hatari ya kudhulumiwa, mradi swala la toba lisihusishwe. Aidha wamesema kuwa watatoa wito kwa makao makuu ya Vatican kulegeza kanuni kuhusu swala la useja.