Kanisa la SDA lapinga uchaguzi wa Jumamosi

Kanisa la wasabato la (SDA) sasa linaitaka tume huru ya uchaguzi na mipaka kuahirisha uchaguzi uliopangiwa siku ya Jumamosi hadi siku nyingine. Kupitia barua kwa mwenyekiti wa tume hiyo A�Wafula Chebukati, viongozi wa kanisa hilo la wasabato hapa nchini walisema kuwa uchaguzi huo unapaswa kuahirishwa hadi siku nyingine ambayo sio Jumamosi na kusema kushindwa kwa tume hiyo kufanya hivyo, kutawanyima mamilioni ya waumini wa kanisa hilo fursa ya kutekeleza haki yao ya kidemokrasia . A�Hatua hiyo inajiri baada ya uchaguzi kukosa kufanyika katika kaunti nne, za Kisumu, Homabay, Siaya na Migori, kutokana na ukosefu wa usalama ulioshuhudiwa katika eneo hilo katika uchaguzi wa hapo jana .

Hata hivyo alipoulizwa kuhusu swala hilo katika mkutano wa awali na wanahabari, Chebukati alisema kuwa hakuna anayelazimishwa kupiga kura na kwamba tume hiyo haiwezi kuongeza muda kupita Jumamosi. Alisema ilani ya uchaguzi wa tarehe 28 Oktoba itatolewa hii leo.