Kanisa katoliki lenye ushawishi mkubwa Congo lajiunga na maandamano dhidi ya Joseph Kabila

 

Kanisa katoliki lenye ushawishi mkubwa katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo limesema kuwa linaunga mkono mgomo wa kitaifa hii leo kutokana na msako mkali kuhusiana na maandamano dhidi ya rais Joseph Kabila. A�Vuguvugu la makundi 10 A�yanashonikiza kuweko kwa demokrasia yametoa wito wa kusitishwa kwa shughuli zote katika miji kuhusiana na vifo vya wanaharakati wawili waliouawa kwa kupigwa risasi na polisi tarehe 25 mwezi Februari. Vifo hivyo viliongeza idadi ya waliofariki kufikia 15 katika maandamano ya desemba 31 na januari 21 kulingana na takwimu za Umoja wa mataifa na kanisa hilo . Kabila alitakiwa kungaa��tuka mamlakani mnamo mwezi Desemba mwaka A�2016, na kutamatisha kupundu chake cha pili mamlakani.
A�