Kampuni za kuuza mafuta zataka bei ya bidhaa hiyo kuongezwa

Kampuni za Mafuta zinataka bei ya Mafuta kuongezwa mwezi ujao katika juhudi za kuhifadhi faida zao.

Kampuni hizo zimedai kwamba zimesalia na asili mia 40 ya Mafuta ambayo hayajauzwa na ambayo yalinunuliwa kwa bei ya juu kabla ya kushuka kwa bei ya bidha hiyo muhimu.

Kwenye barua kwa waziri wa Mafuta  John Munyes, kampuni hizo za Mafuta zilisema kuwa soko la Mafuta lilidorora kutokana na maagizo ya watu kusalia nyumbani pamoja na sheria za kuto-toka nje zilizotangazwa na serikali mwezi jana.

Kampuni hizo za Mafuta zilitoa wito kwa serikali kuishauri halmashauri ya kuthibiti sekta ya kawi kuto-jumuisha shehena ya Mafuta ya mwezi huu iliyonunuliwa kwa bei nafuu katika bei iliyotangazwa hapo awaili ili kuzipa muda wa kuuza Mafuta ambayo hayajauzwa.

Hata hivyo shirikisho la watumiaji bidha nchini  COFEK limekashifu hatua hiyo likisema kuwa kampuni hizo zimedinda kuzingatia hali ya kiuchumi ilivyo nchini,huku zikijali tuu faida zao.