Kampuni za kibinafsi zatafuta njia mpya za kuvutia na kudumisha wateja

Mpango wa hazina ya kitaifa ya bima ya huduma za matibabu (NHIF), umechukua sehemu kubwa ya biashara ya bima za watu binafsi. Hayo ni kulingana na mukurugenzi mkuu wa muungano wa wamiliki wa kampuni za bima nchini- (A.S.K), Tom Gichuhi, ambaye alisema wamiliki hao wa kampuni za bima, sasa wanatafuta njia mpya za kuvutia na kudumisha wateja.

Ripoti ya mwaka 2017 kuhusu biashara ya bima, inaonyesha kwamba biashara hiyo kwa ujumla haijapenya humu nchini, ambapo ilididimia kwa kiwango fulani hadi asilimia 2.71. Kwa upande mwingine, mtaji wa sekta hiyo uliandikisha ukuaji wa asilimia 6.45 hadi shilingi bilioni-209.70 mwaka 2017 kwa kulinganisha na bilioni 197 mwaka 2016. Kitengo cha Bima ya Maisha kiliandikisha ukuaji wa zaidi ya asilimia 40 kufuatia kuimarishwa kwa mbinu za kutafuta masoko mapya na pia kampeini za kuhamasisha umma.

 Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuondoka nchini wiki hii kwenda Beijing, ambako atahudhuria  kongamano la ushirikiano kati ya China na bara Afrika. Wakati wa kongamano hilo, Kenya na China zinatarajiwa kutia saini mkopo wa shilingi bilioni-380 miongoni mwa maswala mengine, kufanikisha ujenzi wa Reli ya kisasa SGR kutoka Naivasha hadi  Kisumu. Mradi wa SGR kati ya Mombasa na Nairobi uligharimu shilingi bilioni 327, huku awamu ya Nairobi hadi Naivasha ya mradi huo ikigharimu shilingi bilioni- 150. Rais Kenyatta alisema kwamba Kenya itaendelea kushirikiana na China ili kuboresha miundo msingi hapa nchini.